Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma anakabiliwa na kadhia nyingine kufuatia ufichuzi kuwa familia ya wafanyabiashara kina Gupta imekuwa ikishawishi siasa za taifa kwa mufa mrefu sana. Umoja wa Ulaya umewawekea vikwazo maafisa tisa wa DRC akiwemo waziri wa mambo ya nje Lambert Mende na mkuu wa idara ya taifa ya ujasusi, kuhusiana na mauaji ya waandamanaji mwaka jana.