MigogoroJamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Ujumbe wa MONUSCO kusalia Kongo kwa mwaka mmoja
21 Desemba 2024Matangazo
Baraza hilo la Usalama la Umoja wa Mataifa limerejesha mamlaka ya kikosi hicho kwa kipindi hicho hata ikiwa ujumbe huo utajiondoa hatua kwa hatua kufuatia ombi la Kinshasa.
Azimio hilo lililopitishwa Ijumaa linasema Baraza hilo linaunga mkono "kujiondoa kwa utaratibu kwa ujumbe wa MONUSCO kulingana na hali ya usalama ya ndani."
Azimio hilo pia limeeleza wasiwasi wake juu ya "kuendelea kwa ghasia mashariki mwa Kongo na mvutano unaoendelea kati yake na Rwanda.
MONUSCO tayari imekamilisha mchakato wa kuondoka huko Kivu Kusini baada ya kufunga ofisi yake mwishoni mwa Juni, lakini wanajeshi wake bado wako Ituri na Kivu Kaskazini.
MONUSCO ina wanajeshi na polisi wapatao 16,000.