SiasaSyria
Blinken afanya ziara nchini Iraq kuhusu hali ya Syria
13 Desemba 2024Matangazo
Blinken amefanya ziara hiyo ya kushtukiza akijaribu kuratibu mikakati ya kikanda kuhusu mustakabali wa Syria kufuatia kupinduliwa kwa rais Bashar al-Assad.
Blinken na al-Sudani watajadili masuala ya ushirikiano na changamoto za usalama wa kikanda, pamoja na mchango wa Marekani katika kufanikisha kipindi cha mpito shirikishi nchini Syria.
Waziri huyo wa mambo ya kigeni wa Marekani amewasili Baghdad akitokea mji mkuu wa Uturuki Ankara alipokutana pia na Rais Tayyip Erdogan ambaye walijadili pia suala hilo na kumueleza umuhimu wa kuwalinda raia wa Syria.