1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUturuki

Blinken amwambia Erdogan "raia wa Syria wanahitaji kulindwa"

13 Desemba 2024

Blinken amemwambia Rais Erdogan kwamba raia wa Syria wanahitaji kulindwa baada ya waasi wa itikadi kali wanaoungwa mkono na Uturuki kuipindua serikali ya Bashar al-Assad.

https://p.dw.com/p/4o5ah
Uturuki | Antony Blinken azungumza na Recep Tayyip Erdoğan
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (kushoto) akizungumza na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan katika uwanja wa ndege wa Esenboga mjini Ankara Uturuki Disemba 12, 2024Picha: Andrew Caballero Reynolds/AP Photo/picture alliance

Blinken alikutana na Rais Erdogan Alhamisi jioni kwa zaidi ya saa moja, kwenye eneo la mapumziko katika uwanja wa ndege wa mji mkuu Ankara, muda mfupi baada ya kiongozi huyo wa Uturuki kumsindikiza waziri mkuu wa Hungary, Viktor Orban aliyekuwa anaondoka nchini humo baada ya ziara yake.

Katika taarifa, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Matthew Miller, amesema Blinken amesisitiza kuhusu umuhimu wa wadau wote nchini Syria kuheshimu haki za binadamu, kuzingatia sheria ya kimataifa ya kibinadamu, na kuchukua hatua zote kuwalinda raia na watu kutoka makundi ya walio wachache.

Kwa upande wake, Rais Erdogan amemwambia Blinken kwamba Uturuki itachukuwa hatua za kinga nchini Syria kwa usalama wake wa kitaifa dhidi ya makundi yote yanayochukuliwa kuwa ya kigaidi.