1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken kutangaza ufadhili zaidi kwa Sudan katika UN

19 Desemba 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, atatangaza katika Umoja wa Mataifa, ufadhili wa ziada kwa ajili ya msaada wa kibinadamu kwa Sudan na za kuzisaidia asasi za kiraia nchini humo.

https://p.dw.com/p/4oLmB
Wakimbizi wa ndani mjini Omdurman
Vita vya wenyewe kwa wenyewe Sudan vimesababisha hali mbaya kabisa ya kibinaadamuPicha: Mohamed Khidir/Xinhua News Agency/picture alliance

Aidha Blinken atatangaza juhudi za kusaidia asasi za kiraia nchini humo, ambako mgogoro umesababisha vifo vya maelfu ya watu na mamilioni kuyahama makazi yao.

Soma pia: Jumuiya ya kimataifa haielewi athari za mgogoro wa Sudan?

Naibu Mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Ned Price, amesema Blinken ataongoza kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Sudan, ambacho kitajikita kwenye msaada wa kibinadamu na ulinzi wa raia.

Mgogoro huo, ulioanza Aprili 2023, ni kati ya Jeshi la Sudan na Kikosi cha Rapid Support Forces (RSF) na umechochea hali mbaya ya kibinadamu, huku mashirika ya Umoja wa Mataifa yakishindwa kutoa msaada ipasavyo.

Marekani inaendelea kushirikiana na washirika wake kuboresha upatikanaji wa msaada na kutafuta suluhisho la kumaliza mapigano kabla ya kumalizika kwa muhula wa Rais Joe Biden mwezi ujao.