MigogoroMashariki ya Kati
Israel yafanya mashambulizi makubwa nchini Syria
10 Desemba 2024Matangazo
Mashambulizi hayo ya Israel yamelenga maeneo zaidi ya 100 ya kijeshi, huku ikichukua udhibiti wa eneo jingine la nchi hiyo. Miito imetolewa na kuitaka Israel kutoifanya operesheni hiyo kuwa endelevu nchini Syria.
Hayo yakiarifiwa, viongozi wa serikali iliyoangushwa nchini Syria wameanza majadiliano ya kukabidhi madaraka kwa njia ya amani, lakini wamesisitiza kuwa hilo linaweza kuchukua siku kadhaa ili kukamilika.
Waziri Mkuu Mohammed Jalali amekutana kwa mazungumzo na Abu Mohammed al-Golani ambaye ndiye kiongozi wa kundi kuu la waasi la Hayat Tahrir al-Sham (HTS), ambalo liliuangusha utawala wa rais wa Syria Bashar al-Assad.