MigogoroMashariki ya Kati
Israel yashambulia maeneo 350 ya kijeshi nchini Syria
11 Desemba 2024Matangazo
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema wimbi la mashambulizi hayo ya anga huko Syria ni muhimu ili kuzuia silaha hizo zisitumike dhidi ya Israel kufuatia kuanguka kwa serikali ya rais Bashar al-Assad.
Katika mji mkuu Damascus, hali imerejea kuwa ya kawaida baada ya sherehe za siku tatu huku maduka na benki vikifunguliwa tena. Waziri Mkuu wa mpito Mohammad al-Bachir ametoa wito wa kudumisha hali ya utulivu.
Marekani imetangaza kuwa itatambua na kuunga mkono serikali mpya ya Syria ambayo itaachana na ugaidi, itatokomeza hifadhi za silaha za kemikali na kulinda haki za walio wachache na wanawake.