Israel yashambulia "njia za kusafirisha silaha" za Hezbollah
6 Desemba 2024Mashambulizi hayo yanatokea wiki moja tu baada ya kufikiwa kwa mpango wa kusitishwa mapigano kati ya Israel na Hezbollah.
Vyombo vya habari vya Lebanon na Syria vimeripoti kuwa shambulio hilo la anga limelenga kivuko cha mpakani cha Al-Arida, eneo ambalo tayari liliharibiwa vibaya wakati wa vita kati ya Israel na Hezbollah.
Israel yalaumiwa katika ripoti mpya ya Amnesty International
Shirika la habari la serikali ya Syria, SANA limeripoti kuwa kivuko hicho cha mpakani cha Al-Arida hakifanyi kazi tena baada ya kushambuliwa leo Ijumaa.
Shambulio hilo limefanyika katikakati ya shutma kutoka pande zote mbili, Israel na Hezbollah, za kukiuka masharti ya makubaliano ya kusitisha mapigano yalioanza kutekelezwa kuanzia Novemba 27, baada ya karibu miezi miwili ya vita kamili kati ya Israel na Hezbollah.