Jeshi la Israel lateketeza hospitali ya Gaza kwa moto
28 Desemba 2024Wanajeshi wa Israeli walivamia na kuchoma moto Hospitali ya Kamal Adwan kaskazini mwa Gaza, baada ya kuwaondoa kwa nguvu wagonjwa na wafanyakazi, Wizara ya Afya ya Gaza imesema, huku jeshi la Israeli likidai hospitali hiyo ilitumika na wapiganaji wa Hamas kama kituo, bila kutoa ushahidi.
Soma pia: Shambulizi la Israel lauwa waandishi watano wa Kipalestina
Jeshi la Israeli lilikanusha kuwajibika moja kwa moja kwa moto mkubwa uliotekeza hospitali hiyo, likisema ni jengo tupu lililoathirika.
Wakati huo huo, mwanamke wa miaka 83 aliuawa kwa kuchomwa kisu na Mpalestina kutoka Ukingo wa Magharibi nchini Israeli, huku jeshi la Israeli likisema limezuia kombora lililorushwa na waasi wa Kihuthi kutoka Yemen, ambao walisema mashambulizi yao hayatakoma mpaka Israel ikubali usitishaji wa mapigano Gaza.