1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChad

Katiba mpya Chad yaidhinishwa kwa asilimia 86

25 Desemba 2023

Tume ya Uchaguzi nchini Chad imetangaza kwamba rasimu ya katiba mpya iliyopigiwa kura wiki moja iliyopita imeidhinishwa kwa asilimia 86.

https://p.dw.com/p/4aYp5
Chad N'Djamena | Kura ya Maoni kuhusu katiba mpya
Tume ya Uchaguzi Chad imesema asilimia 86 ya wapigakura wameridhia rasimu ya katiba mpya.Picha: Denis Sassou Gueipeur/AFP/Getty Images

Hata hivyo, matokeo hayo yamepingwa mara moja na viongozi kadhaa wa upinzani.

Tangazo la tume hiyo limesema idadi ya wapigakura waliojitokeza ilikuwa asilimia 63.75, na kwamba licha ya "hitilafu ndogo" zilizoshuhudiwa, kura hiyo ya maoni ilifanyika vizuri.

Matokeo rasmi ya kura hiyo yatasubiri kuidhinishwa na mahakama ya juu ya taifa hilo mnamo Disemba 28.

Soma pia: Chad yafanya kura ya maoni kuamua kuhusu katiba mpya

Watawala wa kijeshi wa Chad wameipigia upatu rasimu ya katiba iliyopitishwa kuwa hatua muhimu kuelekea kuirejesha Chad chini ya utawala wa kiraia.

Lakini upinzani na wanaharakati wengine wameyapinga madai hayo, na walitoa wito kwa wafuasi wao kuisusia kura hiyo ya maoni iliyofanyika Disemba 17.

Upinzani pia umeyapinga matokeo ya kura hiyo na umesema takwimu zilizotolewa juu ya idadi ya wapiga kura ni za uongo.