1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa Syria asema makundi ya waasi "yatavunjwa"

17 Desemba 2024

Kiongozi wa kundi la kiislamu lililompindua Rais Bashar al-Assad wa Syria amesema kwamba makundi yote ya waasi nchini humo yatavunjwa na wapiganaji wake watawekwa chini ya usimamizi wa wizara ya ulinzi.

https://p.dw.com/p/4oEAz
Abu Mohammed al-Jolani
Abu Mohammed al-Jolani.Picha: Aref Tammawi/AFP/Getty Images

Abu Mohammed al-Jolani, mkuu wa kundi la waasi la Hayat Tahrir al-Sham(HTS) lililochukua madaraka nchini Syria mwanzoni mwa mwezi Disemba amesema mchakato huo utafanyika kisheria na wapiganaji hao watapatiwa mafunzo na kupandisha vyeo chini ya kanuni za wizara ya ulinzi.

Kiongozi huyo pia ametoa rai ya kuwepo umoja nchini humo baina ya makundi tofauti ya kidini na kikabila na kusisitza kwamba "Syria ni lazima ibakie kuwa taifa lililoungana".

Katika hatua nyingine al-Jolani anayefahamika pia kwa majina ya Ahmed al-Sharaa ametoa mwito wa kuondolewa vikwazo vyote dhidi ya Syria ili kuwezesha wakimbizi wa nchi hiyo kurejea nyumbani.

Ametoa matamshi hayo alipokutana kwa mara ya pili na ujumbe wa wanadiplomasia wa Uingereza wanaoitembelea Syria.