Kiongozi wa upinzani Msumbuji asema polisi wanahimiza vurugu
26 Desemba 2024Mondlane amesema kwenye mitandao ya kijamii kuwa maandamano yao yanalilenga Baraza la Kikatiba, tume ya uchaguzi na chama cha Frelimo chenyewe, taasisi ambazo anasema zilihusika na udanganyifu.
Amesema hakuna hatua yoyote inayochukuliwa na polisi dhidi ya waporaji, akiongeza kuwa ni kama wanawahimiza watu kushambulia na kuiba.
Soma pia: Baraza la katiba Msumbiji yathibitsiha ushindi wa chama tawala cha Frelimo
Mahakama ya Kikatiba ya nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika ilithibitisha Jumatatu kuwa Frelimo, ambao wamekuwa madarakani tangu uhuru kutoka kwa Ureno mwaka wa 1975, walishinda uchaguzi wa rais Oktoba 9 ambao ulizusha machafuko. Mashirika ya kiraia yanasema watu 150 wameuawa mpaka sasa. Hapo jana, wafungwa 1,000 walitumia fursa ya ghasia hizo na kutoroka jela moja la ulinzi mkali mjini Maputo.