Wanaeshi 1100 wa K. Kaskazini wauawa au kujeruhiwa Ukraine
23 Desemba 2024Idadi hiyo mpya inafuatia ripoti ya shirika la kijasusi la Seoul ya wiki iliyopita, ambayo ilisema takriban wanajeshi 100 wa Korea Kaskazini wameuawa tangu waingie vitani mwezi Disemba. Korea Kaskazini imetuma maelfu ya wanajeshi ili kuimarisha jeshi la Urusi, ikiwa ni pamoja na kwenye eneo la mpakani la Kursk ambalo lilikuwa chini ya udhibiti wa vikosi vya Ukraine mapema mwaka huu. Taarifa hiyo ya Korea Kusini inasema kupitia vyanzo vyao mbalimbali vya kijasusi vinatathmini kwamba wanajeshi 1,100 wa Korea Kaskazini ambao hivi karibuni wamepigana na vikosi vya Ukraine wameuawa ama kujeruhiwa. Korea Kaskazini na Urusi zimeimarisha uhusiano wao wa kijeshi tangu uvamizi wa Moscow nchini Ukraine mnamo Februari 2022 huku mkataba wa kihistoria wa ulinzi kati ya Pyongyang na Moscow, uliotiwa saini mwezi Juni umeanza kutekelezwa mapema mwezi huu.