Macron kutembelea Mayotte kilichoharibiwa na Kimbunga Chido
17 Desemba 2024Matangazo
Kupitia ukurasa wake wa X, Macron alisema atakitembelea kisiwa hicho ndani ya siku kadhaa zijazo, kuwaunga mkono raia wake, maafisa na mashirika ya kutoa huduma muhimu. Macron pia alisema anapanga kutangaza kipindi cha maombolezo cha kitaifa. Hadi sasa serikali imetangaza vifo vya watu 21 huku zaidi ya watu 1,400 kujeruhiwa vibaya kutokana na kimbunga hicho, kilichopiga eneo hilo lililochini ya Ufaransa na kusababisha uharibifu wa majengo, miundombinu ya nishati na mawasiliano Wakoaji wanaendelea na juhudi za kuwafuta manusura na kurejesha huduma muhimu huko.