1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVenezuela

Maduro atangaza kukamatwa 'mamluki' wakiwemo Wamarekani

8 Januari 2025

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela ametangaza kukamatwa kwa wale aliowaita "mamluki" saba, wakiwemo raia wawili wa Marekani, aliosema ni wa maafisa wa ngazi za juu.

https://p.dw.com/p/4ovaF
Maduro Venezuela
Rais Nicolas Maduro wa Venezuela.Picha: Java

Kwa mujibu wa Rais Maduro, miongoni mwa waliokamatwa ni raia wawili wa Colombia na watatu wa Ukraine, ambao alidai waliingia nchini Venezuela kwa lengo la kufanya matendo ya kigaidi.

Hayo yakijiri, kiongozi wa upinzani wa Venezuela anayeishi uhamishoni, Edmundo Gonzalez, amesema mkwe wake wa kiume ametekwa katika mji mkuu, Caracas, hapo jana.

Soma zaidi: Kiongozi wa upinzani aapa kuzuia mipango ya Maduro ya kuapishwa madarakani

Mwanasiasa huyo ambaye yuko ziarani nchini Marekani kusaka uungwaji mkono dhidi ya Maduro, ameandika kupitia mtandao wa X kwamba mkwe wake huyo, Rafael Tudares, alitekwa wakati akielekea kuwashusha wajukuu wawili wa Gonzalez.

Bado haijafahamika ikiwa mkwe wa Gonzalez na wajukuu zake ni sehemu ya waliotangazwa kukamatwa na Maduro.

Maduro anatazamia kuapishwa kwa muhula wa tatu wa miaka sita hapo Ijumaa.