1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu Nambia waendelea kupiga kura baada ya zoezi kufungwa

28 Novemba 2024

Maelfu ya Wanamibia walikumbana na ucheleweshaji mkubwa wa kupiga kura katika uchaguzi muhimu kutokana na changamoto za uratibu jana Jumatano.

https://p.dw.com/p/4nVS7
Namibia | Uchaguzi
Changamoto za uratibu na miundombinu vilichelewesha zoezi la upigaji kura kukamilika kwa wakati.Picha: Simon Maina/AFP/Getty Images

Maelfu ya Wanamibia walikumbana na ucheleweshaji mkubwa wa kupiga kura katika uchaguzi muhimu kutokana na changamoto za uratibu jana Jumatano, huku chama tawala cha SWAPO kikikabiliwa na changamoto kubwa zaidi kwa utawala wake wa miaka 34.

Licha ya baadhi ya wapiga kura kusubiri hadi masaa 12 kutokana na matatizo ya kiufundi, sheria za uchaguzi zilihakikisha kwamba bado wangeweza kupiga kura baada ya muda uliopangwa kumalizika.

Soma pia: Raia wa Namibia wapiga kura kumchagua Rais

Chama kikuu cha upinzani, IPC, kiiiishutumu tume ya uchaguzi kwa makusudi ya kuzuia wapiga kura, wakati mgombea wa SWAPO, Netumbo Nandi-Ndaitwah, alihimiza watu kujitokeza kwa wingi.

Malalamiko kuhusu ukosefu wa ajira na ukosefu wa usawa yanaweza kusababisha duru ya pili ya kupiga kura kwa mara ya kwanza, huku hasira za vijana zikiongezeka katikati ya ukosefu mkubwa wa ajira.

Wachambuzi wanasema duru ya pili sasa ni uwezekano halisi kwa mara ya kwanza katika historia ya Namibia.