Makundi ya waasi Syria yakubali kuweka chini silaha
24 Desemba 2024Matangazo
Viongozi wa makundi kadhaa ya waasi yamekubali hatua hiyo baada ya kuwa na mkutano na kiongozi mpya wa Syria, Ahmed al-Sharaa. Al-Sharaa ambaye zamani alijulikana kama Abu Mohammed al-Joulani - aliweka wazi kuwa hatokubali makundi yaliyojihami kufanya shughuli zao nje ya udhibiti wa serikali. Kundi lake la waasi la Hayat Tahrir al-Sham liliunda serikali ya mpito baada ya kuuangusha utawala wa Bashar al Assadmnamo Desemba 8. Syria imegawika tangu kuzuka kwa maandamano ya kuipinga serikali ya mwaka 2011 na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.