Matokeo ya urais DRC kutolewa baada ya masaa 48
7 Desemba 2011Matangazo
Maafisa nchini humo wamedai wanahitaji muda mwingine zaidi ili kuweza kukukusanya matokeo ya mwisho, baada ya kutokea makosa katika usimamizi. Kutokana na hali hiyo matokeo kamili kwa hivi sasa yatategemewa alhamis jioni. Rais wa sasa Joseph Kabila mpaka sasa anaongoza kwa asilimia 46.4 ya kura katika theluthi mbili ya kura zilizoripotiwa kuhesabiwa. Mpinzani wake mkubwa Etienne Tshisekedi anamfuatia kwa asilimia 36.2. Vurugu za uchaguzi nchini humo zimesababisha vifo vya watu 18 na kujeruhiwa zaidi ya 100. Kwa mujibu wa makundi ya haki za binadamu vifo vingi vimetokana na jeshi la serikali.