Matokeo ya urais DRC yanatarajiwa kutolewa leo
8 Desemba 2011Matangazo
Polisi wamejiandaa kikamilifu na kiasi cha wanajeshi 20,000 wamejiweka tayari katika mji wa Kinshasa, eneo ambalo jana wafuasi wa upinzani wameonekana wakiwarushiwa mawe polisi na wao kujibu kwa mabomu ya kutoa machozi. Rais wa sasa Joseph Kabila amepata asilimia 49 ya kura, kwa mujibu wa asilimia 89 ya vituo vya kupigia kura. Kiongozi wa Upinzani Etienne Tshisekedi anafuatia kwa kura asilimia 33. Kuchelewa kwa vifaa kumesababisha maafisa kuongeza muda wa kumtangaza mshindi kwa masaa 48 zaidi ya muda wa kikatiba wa rais Kabila kuwepo madarakani. Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutolewa hii leo.