You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Uchaguzi Mkuu wa Ujerumani 2025
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
Michezo
Pata habari na uchambuzi wa michezo.
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Bundesliga: Bayern Munich wawinda kipa mwingine
Kocha wa Bayern Munich Julian Nagelsmann amesema klabu hiyo inataka kumsajili mlinda mlango mwingine kufuatia majeraha aliyoyapata nahodha wa kikosi cha Ujerumani na kipa wa klabu hiyo Manuel Neuer. Je wataweza kutimiza malengo yao katika dirisha dogo la usajili? Swai hilo analijibu Josephat Charo kutoka dawati la Michezo.
Frankfurt haitamuuza Randal Kolo Muani
Mkurugenzi wa michezo wa Eintracht Frankfurt Markus Krösche amesema hawatawauza wachezaji muhimu kama vile Randal Kolo Muani. Dani Olmo wa RB Leipzig ana mipango ya kurejea kwao Uhispania siku za usoni. Na De Ligt anataka kung'ara na klabu yake ya Bayern Munich. Kwa haya na mengine yanayoendelea katika Bundesliga msikilize Josephat Charo akihojiwa na Saumu Njama.
DW Michezo: Ureno yamteua Martinez kuwa kocha mkuu
Dortmund yapigwa jeki na kurejea kwa nahodha Marco Reus na Sebastian Haller. Rais wa shirikisho la kandanda Ufaransa ajikuta kikaangoni kufuatia kauli zake kuhusu Zidane na miamba yaondolewa katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar.
Polter kukosekana Schalke kwa miezi kadhaa
Mshambuliaji wa klabu ya Schalke Sebastian Polter huenda akawa nje ya uwanja kwa miezi kadhaa kutokana na jeraha baya alilolipata kwenye goti katika mechi ya kirafiki na FC Zurich ya Uswisi. Jitihada za Schalke kujinasua mkiani mwa Bundesliga zitaathirika vipi? Msikilize Josephat Charo akihojiwa na Naomi William.
Gladbach haitamuuza Sommer kwa Bayern
Klabu ya Borussia Moenchengladbach imesema haitamuuza mlindamlango Yann Sommer kwa mabingwa watetezi wa Bundesliga Bayern Munich. Juhudi za Bayern kulijaza pengo la Manuel Neuer bado ziko mashakani. Sikiliza mahojiano kati ya Naomi William na Josephat Charo wa dawati la michezo la DW Kiswahili.
Josko Gvardiol kutafakari hatima yake Leipzig
Beki ya klabu ya RB Leipzig na timu ya taifa ya Croatia Josko Gvardiol amesema atatafakari kuhusu mustakbali wake na klabu hiyo msimu huu wa sitini wa Bundesliga utakapokamilika.
Bayern Munich kumsaini beki wa Uholanzi Daley Blind
Gazeti la michezo la Bild limeripoti kuwa mazungumzo kati ya Bayern na Blind yalianza kati ya Krismasi na Mwaka mpya.
Klabu za Bundesliga zakimbizana na dirisha dogo
Klabu zinazoshiriki ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani Bundesliga, zinaendelea na dirisha dogo la usajili, huku klabu ya Cologne ikifanikiwa kumwaga wino kwa kinda Linton Maina mwenye asili ya Kenya. Sylvia Mwehozi amezungumza na Josephat Charo kutoka dawati la Michezo.
Davie Selke wa Hertha Berlin ahamia Cologne
Mshambuliaji wa Hertha Berlin Davie Selke amejiunga na klabu ya Cologne kwa uhamisho huru. Selke hakufanikiwa sana msimu huu na klabu ya Hertha ambako alikuwa akicheza kwa mkopo na akarudishwa timu yake ya zamani Werder Bremen. Sikiliza mahojiano kati ya Saumu Mwasimba na Josephat Charo kuhusu kinachoendelea katika Bundesliga.
Je, utamkumbuka vipi Pele?
Umahiri wa Pele utaendelea, mbwembwe na madoido ni huoongeza burudani la kandanda
Brazil yajiandaa na mazishi ya Pele
Rais wa Brazil Lula da Silva ataongoza shughuli hiyo ya mazishi huko Santos
Leipzig waelekea Abu Dhabi kwa mazoezi
Ronaldo kuzinduliwa na klabu yake mpya ya Al Nassr, Saudi Arabia. Dar Young Africans yapepea kileleni mwa ligi
Ulimwengu wamuaga mwanasoka maarufu Pele
Pele atazikwa Jumanne (03.01.2023).
Marco Rose tumbo joto na safu yake ya ulinzi
Ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani Bundesliga inatarajiwa kurejea viwanjani Ijumaa Janauri 20 kwa pambano kati ya RB Leipzig na mabingwa watetezi Bayern Munich. Grace Kabogo na Josephat Charo wazungumzia duru ya pili ya Bundesliga na mengineyo katika michezo.
Matukio ya mwaka 2022 katika michezo
Kombe la Dunia, Ligi ya Mabingwa Ulaya, mashindano ya riadha, mwaka huu unaokamilika ulikuwa na mambo lukuki kwa mashabiki wa michezo, ambapo pia rekodi za zamani zilivunjwa na mpya zikaandikwa. Karibu katika Makala hii maalum ya matukio muhimu yaliyogonga vichwa vya Habari za michezo katika mwaka wa 2022
Mashabiki wasubiri Bundesliga kwa hamu
Mashabiki wa soka Ujerumani wanasubiri kwa hamu na ghamu kuanza tena kwa ligi kuu ya Bundesliga Januari 20. Timu zinalazimika kusubiri kwa muda mrefu kabla kuanza kucheza tena baada ya michuano ya kombe la dunia. Mashabiki wana hamu kubwa kuwaona wachezaji wakirejea viwanjani. Sikiliza mahojiano ya Naomi William na Josephat Charo.
Gwiji wa soka Pele aaga dunia akiwa na umri wa miaka 82
Pele alifunga mabao 1,281 katika mechi 1,363 katika muda wa miaka 21, ikiwemo mabao 77 katika mechi 92 akiichezea Brazil
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 10 wa 10
Ukurasa unaofuatia