Mjumbe wa UN aonya dhidi ya kuanguka taasisi za Syria
14 Desemba 2024Matangazo
Pedersen ameyasema hayo leo wakati ambapo wanadiplomasia wanakutana Jordan kuujadili mzozo wa Syria. Pia ameunga mkono mchakato wa kisiasa ulio ''thabiti, wa kuaminika na unaowajumuisha wote'' katika kuunda serikali ijayo, wakati alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani,Antony Blinken. Amesema wanahitaji kuhakikisha kuwa taasisi za serikali haziporomoki, na wanapata msaada wa kiutu haraka iwezekanavyo. Amesema iwapo hilo litafanikiwa, pengine kutakuwa na fursa mpya kwa watu wa Syria. Wanadiplomasia wa ngazi ya juu wa nchi za Kiarabu, Uturuki, Umoja wa Ulaya na Marekani, wanakutana katika mji wa Jordan, Aqaba, chini ya wiki moja tangu waasi walipouondoa utawala wa Assad.