MigogoroSyria
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa ataka Syria iondolewe vikwazo
15 Desemba 2024Matangazo
Pedersen, amesema wakati wa ziara yake mjini Damascus kuwa ni muhimu kuona vikwazo vikiondolewa haraka ili kuruhusu juhudi za kuijenga upya Syria.
Serikali ya Syria imekabiliwa na vikwazo vikali vya Marekani, Umoja wa Ulaya na mataifa mengine kwa miaka mingi kutokana na ukandamizaji wa Assad dhidi ya maandamano ya amani yaliyotokea mwaka 2011, ambayo yaligeuka na kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Katika hatua nyingine, zaidi ya wahamiaji 7,600 wa Syria walivuka mpaka wa Uturuki kurejea nyumbani katika muda wa siku tano baada ya kuangushwa kwa mtawala wa Assad, hii ikiwa ni kulingana na Waziri wa mambo ya ndani wa Uturuki mapema leo.