1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa NATO amkingia kifua Kansela Scholz

23 Desemba 2024

Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya nchi za magharibi, NATO, Mark Rutte amesema ukosoaji mkali wa hivi karibuni wa rais Zelensky wa Ukraine kwa Kansela wa Ujerumani Olaf Schoz hauna msingi.

https://p.dw.com/p/4oWO4
Belgien Treffen von NATO-Generalsekretär Mark Rutte und Wolodymyr Selenskyj in Brüssel
Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte, kulia, akipeana mkono na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy kabla ya mkutano huko Brussels Jumatano, Dec. 18, 2024.Picha: Olivier Matthys, Pool Photo via AP/picture alliance

Hivi majuzi Zelensky alimkosoa Scholz kwa kitendo chake cha kuzungumza na rais wa Urusi Vladmir Putin kinyume na matakwa yake. Zelensky mara zote amekuwa akisisitiza kupatiwa makombora ya Taurus yaliyotengenezwa nchini Ujerumani na yenye uwezo wa kupiga maeneo makubwa ya Urusi. Mark Rutte amesisitiza kwamba makombora hayo yanaweza kuisaidia Ukraine katika vita vyake lakini suala hilo linabaki kuwa maamuzi ya Ujerumani kuamua kutoa vifaa hivyo vya kijeshi ama la. Scholz amekataa kutoa vifaa hivyo bila kujali maamuzi yaliyochukuliwa na washirika wenzake wa NATO akisema kwamba hatua hiyo inaweza kuleta hatari zaidi ya kutanuka kwa vita hivyo.