Mlinda amani wa Rwanda auawa Afrika ya Kati
11 Julai 2023Taarifa ya Umoja wa Mataifa imesema washambuliaji watatu wameuawa na mmoja amekamatwa baada ya mashambulizi hayo ya siku ya Jumatatu (Julai 10).
Hadi sasa, hakuna kundi lolote la wanamgambo lililoshutumiwa kuhusika na mashambulizi hayo.
Ghasia zilipungua nchini humo baada ya kusainiwa makubaliano ya amani kati ya serikali na vikundi 14 vyenye silaha mnamo mwezi Februari 2019, lakini hali bado ni tete kwani maeneo mengi bado yapo nje ya udhibiti wa serikali.
Soma zaidi: Rwanda imetuma wanajeshi 300 kujiunga na MINUSCA, Bangui
UN yalaani machafuko Jamhuri ya Afrika ya Kati
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa walitumwa Jamhuri ya Afrika ya Kati mnamo mwaka 2014 ili kusaidia kutuliza ghasia zilizozuka mwaka mmoja baada ya waasi wa Seleka - wengi wao kutoka jamii ya Waislamu - kumuondoa madarakani aliyekuwa rais wa wakati huo, Francois Bozize, jambo lililopelekea mashambulizi ya kulipiza kisasi kutoka kwa wanamgambo wengi wa Kikristo.