1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NAIROBI : Mke wa mtuhumiwa wa Al Qaeda aachiwa

27 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBxx

Mke wa mmojawapo wa wanachama wa Al Qaeda wa Afrika anayesakwa kwa udi na uvumba ameachiliwa huru nchini Ethiopia baada ya kukamatwa wakati akijaribu kuondoka Somalia wakati wa mapigano ya mwaka mpya nchini humo.

Alamin Kimanthi Mwenyekiti wa Chama cha Haki za Binaadamu cha Waislamu nchini Kenya ameliambia shirika la habari la Uingereza Reuters kwamba Halima Badroudine ameachiliwa na watoto wake pamoja na watu wengine saba.

Mume wake Fazul Abdullah Mohammed yuko katika orodha ya magaidi wanaosakwa mno na shirika la upelelezi la Marekani FBI na imetolewa zawadi ya dola milioni 5 kwa habari zitakazopelekea kukamatwa kwake.

Mtuhumiwa huyo mzalia wa Comoro anadaiwa kuhusika na uripuaji wa mabomu hapo mwaka 1988 katika balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania ambapo watu 240 waliuwawa.