1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Namibia yarefusha muda wa upigaji baada ya shida za uratibu

28 Novemba 2024

Wanamibia waliendelea kupiga kura mapema, baada ya kukumbana na ucheleweshaji mkubwa katika uchaguzi huo muhimu kutokana na changamoto za uratibu.

https://p.dw.com/p/4nWEY
Namibia | Uchaguzi
Namibia yarefusha muda wa upigaji kura kutokana na changamoto za uratibuPicha: Simon Maina/AFP/Getty Images

Zoezi la kuhesabu kura lilikuwa limeanza katika baadhi ya vituo huku matokeo ya awali yakitarajiwa kutangazwa ifikapo Jumamosi kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi.

Kutokana na ukosoaji kutoka kwa vyama vya kisiasa na wapiga kura kuhusiana na mistari hiyo mirefu, Tume ya Uchaguzi ya Namibia - ECN ililazimika kurefusha saa za upigaji kura.

Namibia yapiga kura huku chama tawala kikikabiliwa na kinyang'anyiro kikali

Chama tawala cha SWAPO kinakabiliwa na changamoto kubwa zaidi kwa utawala wake wa miaka 34. Chama kikuu cha upinzani, Idependent Patriots for Change IPC, kiliishutumu tume ya uchaguzi kwa makusudi ya kuwazuia wapiga kura, wakati mgombea wa SWAPO, Netumbo Nandi-Ndaitwah, alihimiza watu kujitokeza kwa wingi.

Malalamiko kuhusu ukosefu wa ajira na ukosefu wa usawa yanaweza kusababisha duru ya pili ya kupiga kura kwa mara ya kwanza, huku hasira za vijana zikiongezeka katikati ya ukosefu mkubwa wa ajira. Wachambuzi wanasema duru ya pili sasa ni uwezekano halisi kwa mara ya kwanza katika historia ya Namibia.