Migogoro
Polisi 14 wa Syria wauawa katika shambulio ka kuvizia Tartus
26 Desemba 2024Matangazo
Maafisa 14 wa polisi wa Syria wameuawa na wengine 10 kujeruhiwa katika shambulio la kuvizia lililofanywa na wafuasi wa utawala wa Assad katika mkoa wa Tartous.
Waziri mpya wa Mambo ya Ndani ameahidi kuchukua hatua kali dhidi ya wale wanaotishia usalama wa Syria au kuhatarisha maisha ya raia wake.
Wakati huo huo, polisi imetangaza kafyu ya usiku kucha katika mji wa Homs kufuatia machafuko yaliyochochewa na maandamano ya jamii za wachache wa Alawi na Mashia, ambayo yamekuwa sehemu ya machafuko makubwa zaidi tangu kuondolewa kwa Assad zaidi ya wiki mbili zilizopita.