1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Pakistan imeachana na jaribio lake la kumkamata Khan

15 Machi 2023

Polisi nchini Pakistan imeachana na jaribio lake la kumkamata waziri mkuu wa zamani Imran Khan, kwa kukomesha mzingiro wa makazi yake baada ya makabiliano ya vurugu na mamia ya wafuasi wake.

https://p.dw.com/p/4OifH
Pakistan Ausschreitungen in Lahore
Picha: Arif Ali/AFP

Mahakama Kuu ya Lahore iliwaamrisha maafisa kusitisha operesheni hiyo na kutomkamata Khan hadi kesho saa nne asubuhi.

Msaidizi wa Khan, Fawad Chaudry amesema mahakama itaendelea kesho na vikao vya kusikiliza suala hilo.

Polisi walipambana na wafuasi wa Khan usiku kucha, ikiyatua mambomu ya kutoa machozi na kukwepa mawe yaliorushwa na makundi yenye hasira.

soma pia:Khan: Hakuna nafasi tena ya kutetereka

Waandishi habari na mashuhuda karibu na nyumbani kwa Khan, katika kiunga cha Lohore cha Zaman Park, wamesema polisi na mgambo wamerudi nyuma baada ya kutekeleza vizuwizi na vituo vya ukaguzi walivyokuwa wameweka.

Khan aliondolewa madarakani kupitia kura ya kutokuwa na imani naye mwaka jana, na amefunguliwa kesi kadhaa wakati akipiga kampeni ya kuitisha uchaguzi wa mapema.

Kurasa rasmi za chama chake cha Pakistan Tareek - e-Insaf, PTI, zimechapisha vidio zinazomuonyesha Khan akiwa ndani ya bustan yake, na wafuasi wenye furaha wakisherehekea nje.