JamiiAfrika Kusini
Zoezi la uokoaji lakamilika katika mgodi wa Stilfotein
16 Januari 2025Matangazo
Takriban wachimba migodi 78 wamethibitishwa kufariki huku manusura 246 wakiokolewa. Makundi ya kutetea haki za binaadamu nchini Afrika Kusini yamesema kuwa idadi ya vifo inaweza kuwa kubwa zaidi na kwamba waathiriwa wanashukiwa kuwa walifariki kwa njaa au upungufu wa maji mwilini, ingawa mamlaka hawajatoa sababu zilizopelekea vifo hivyo.
Soma pia: Takriban watu 100 wafariki, mamia wakwama mgodini Afrika Kusini
Polisi hata hivyo wamesema wanaamini kuwa wamefanikiwa kuwaondoa manusura waliosalia na kuopoa miili yote baada ya mamia ya wachimba migodi kukwama kwa miezi kadhaa katika mgodi huo wenye kina kirefu wakifanya kazi kinyume cha sheria.