Raia wa Syria washerehekea kuanguka utawala wa Assad
9 Desemba 2024Matangazo
Assad alikimbilia Urusi jana Jumapili baada ya mashambulizi yaliyoongozwa na waasi walioudhibiti mji mkuu huo na hatimae kufungua ukurasa mpya katika historia ya Syria baada ya miongo mitano ya utawala wa ukoo wa Assad.
Bashar al-Assad amepewa hifadhi nchini Urusi kutokana na kilichoelezwa kuwa sababu za kibinaadamu. Rais wa Marekani Joe Biden amesema ni lazima Assad awajibishwe kwa vitendo vya mauaji na mateso ya maelfu ya Wasyria.
Wakati huo huo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kufanya mkutano wa dharura na wa faragha ili kuijadili hali inayoendelea nchini Syria.