Syria iache kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji
17 Novemba 2011Matangazo
Syria, imeonywa na umoja huo kuwa itawekewa vikwazo vya kiuchumi, isipochukua hatua hizo. Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za kiarabu mjini Rabat, Morocco umethibitisha kuwa Syria imetengwa kutoka kundi hilo la kiarabu, kwa muda usiojulikana.
Hatua zinazozidi kuitenga serikali ya Rais wa Syria Bashar al-Assad, zimewapa moyo wanajeshi wa Syria walioasi. Imeripotiwa kuwa wanajeshi hao wameshambulia jengo la ofisi ya idara ya upelelezi, ya jeshi la anga mjini Harasta nje ya mji mkuu Damascus. Vile vile wamekishambulia kituo kimoja cha ukaguzi wilayani Hama. Waasi wa kundi linaloitwa jeshi huru la Syria, wamelichagua baraza la kijeshi kwa azma ya kumpindua Rais Assad.