1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroNigeria

Takriban watu 10 wauawa kimakosa na jeshi Nigeria

27 Desemba 2024

Watu wapatao 10 waliuawa kimakosa wakati ndege ya jeshi la Nigeria iliyokuwa inawafuatilia majambazi katika vijiji viwili ilipowashambulia katika jimbo la kaskazini magharibi la Sokoto.

https://p.dw.com/p/4ocQS
Watu 10 wauawa kimakosa katika operesheni ya kijeshi Nigeria
Watu 10 wauawa kimakosa katika operesheni ya kijeshi NigeriaPicha: AP/dpa/picture alliance

Watu wapatao 10 waliuawa kimakosa wakati ndege ya jeshi la Nigeria iliyokuwa inawafuatilia majambazi katika vijiji viwili ilipowashambulia katika jimbo la kaskazini magharibi la Sokoto.

Gavana wa jimbo hilo Ahmed Aliyu amesema raia wengine kadhaa walijeruhiwa kwenye mkasa huo.

Amesema ieshi lilikuwa na dhamira ya kupambana na makundi ya wahalifu wenye silaha lakini waliwapiga mabomu kimakosa watu wasio na hatia.

Gavana huyo ameongeza kuwa serikali itashirikiana na mamlaka zingine kuchunguza operesheni ya kijeshi iliyosababisha vifo vya watu kwenye vijiji viwili vya Gidan Sama na Rintuwa kwenye jmbo hilo la Sokoto la magharibi mwa Nigeria.