1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Ukraine yazishambulia Moscow, Crimea

25 Agosti 2023

Urusi imesema kuwa Ukraine imerusha makombora kuelekea mji mkuu wake, Moscow, na kulishambulia eneo la Crimea linalokaliwa kimabavu na Urusi kwa ndege 42 zisizo na rubani.

https://p.dw.com/p/4VZHw
Rauch an der Kertsch-Brücke
Picha: Alyona Popova/TASS/dpa/picture alliance

Hilo ni mojawapo ya mashambulizi makubwa zaidi ya angani ya Ukraine kuwahi kufanyika katika ardhi inayoshikiliwa an Urusi.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi inasema kiombora la S-200 limedunguliwa katika eneo la Kaluga linalopakana na Moscow.

Gavana wa Kaluga, Vladislav Shapsha, amesema hakuna waliouwawa katika shambulizi hilo.

Soma: Moscow: Ukraine ilijaribu kuharibu daraja la Crimea

Ukraine haijatoa tamko kuhusiana na ripoti hizo na kwa kawaida haikubali kuhusika na mashambulizi ndani ya Urusi au katika maeneo yanayodhibitiwa na Urusi nchini Ukraine.

Mashambulizi hayo ya hivi karibuni ni ongezeko la matukio kama hayo ambayo yamekuwa yakiripotiwa baada ya droni mbili kudunguliwa karibu na ikulu ya Kremlin mapema mwezi Mei.