Urusi yaushambulia mji mkuu wa Ukraine, watu watatu wauawa
18 Januari 2025Urusi imefanya mashambulizi ya droni na makombora katika mji mkuu wa Ukraine mapema leo. Mkuu wa kijeshi wa mji wa Kyiv, Timur Tkachenko, amesema watu watatu wameuawa kwenye mashambulizi hayo.
Meya wa mji wa Kyiv, Vitalii Klitschko amethibitisha mashambulizi hayo ya Urusi akisema kwamba yamesababisha uharibifu katika baadhi ya majengo na baadhi ya vituo.
Soma zaidi. Viongozi wa Urusi na Iran wasaini mkataba wa ushirikiano wa kimkakati
Kwa upande mwingine jeshi la anga vya Ukraine limeripoti kwamba limezidungua droni 24 na mabomu mawili yaliyorushwa na vikosi vya Urusi usiku wa kuamkia leo.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa jumla ya droni 39 na mabomu manne yalirushwa katika maeneo mbalimbali ya Ukraine. Vita vya Urusi nchini Ukraine vyenye karibu miaka mitatu bado vimeendelea kuchukua sura mpya kila uchao.