1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Vanuatu yakabiliwa na tetemeko kubwa la ardhi

22 Desemba 2024

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.1 katika kipimo cha Richter limetokea katika ufuo wa Vanuatu mapema Jumapili, Shirika la Utafiti wa Jiolojia la Marekani limesema.

https://p.dw.com/p/4oTr4
Vanuatu
Picha ikionyesha uharibifu uliofanywa na tetemeko la ardhi nchini VanuatuPicha: AFP

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.1 katika kipimo cha Richter  limetokea katika ufuo wa Vanuatu mapema Jumapili, Shirika la Utafiti wa Jiolojia la Marekani limesema. Tetemeko hilo limetokea siku chache baada ya tetemeko lingine la ukubwa wa kipimo cha richter 7.3  kupiga karibu na kisiwa hicho katika visiwa vya Pasifiki.

Kisiwa kikuu cha taifa hilo, Efate, bado kinakabiliana na athari za tetemeko la ardhi lililopiga siku ya Jumanne lililouwa watu kumi na mbili mpaka sasa huku majengo pia yakianguka na kupelekea maporomoko ya ardhi katika mji huo.

Soma zaidi.Tetemeko la ardhi lawaua watu 14 kisiwa cha Vanuatu 

Taifa hilo la Kusini mwa bahari ya Pasifiki lilitangaza hali ya dharura kwa  siku saba na amri ya kutotoka nje usiku kufuatia tetemeko la kwanza. Taarifa za Umoja wa Mataifa zinasema zaidi ya watu 1,000 wameyakimbia makazi kutokana na tetemeko hilo ingawa wengi wao wako katika vituo vya uokozi.

Taifa la Vanuatu lenye wakaazi 320,000 lina mjumuisho wa visiwa kadhaa vidogo vidogo liko katika eneo linalokabiliwa na matetemeko ya ardhi mara kwa mara katika Bahari ya Pasifiki.