1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiVenezuela

Venezuela yautoza faini ya dola milioni 10 mtandao wa TikTok

Saleh Mwanamilongo
31 Desemba 2024

Maafisa wa nchi hiyo walihusisha vifo vya watoto watatu waliofariki baada ya kunywa kemikali kufuatia vidio zilizochapishwa kwenye mtandao wa TikTok.

https://p.dw.com/p/4ohdW
Mahakama kuu ya Venezuela yatoza faini ya dola milioni 10 kwa mtandao wa TikTok
Mahakama kuu ya Venezuela yatoza faini ya dola milioni 10 kwa mtandao wa TikTokPicha: Dan Kitwood/Getty Images

Mtandao huo maarufu wa kijamii unaochapisha video fupi umeagizwa pia kufungua ofisi zake nchini Venezuela. Kwa mujibu wa mahakama ya nchi hiyo ni kwamba fedha hizo zitatumika "kuunda hazina ya waathiriwa wa mtandao wa TikTok."

Mnamo Novemba, Rais wa Venezuela Nicolas Maduro alitishia kuchukuwa "hatua kali" dhidi ya mtandao wa TikTok ikiwa usingeliondowa maudhui yanayohusiana na kile alichokiita "mashindano ya uhalifu."

Umaarufu wa kimataifa wa mtandao huo wa Kichina unatokana na mashindano yake kama hayo. Lakini mtandao huo umekabiliwa na shutuma kwa kuwaweka watumiaji hatarini kwa kuruhusu kuenea kwa video hatari za mashindano.