Viongozi wa EU watahadharisha kuhusu mustakabali wa Syria
19 Desemba 2024Kundi la Kiislamu la Hayat Tahrir al-Sham (HTS), ambalo limekuwa na jukumu kubwa katika kumuondoa al-Assad, limedai kuwa linataka kuwakilisha Syria nzima. De Croo amesema Umoja wa Ulaya unapaswa kuwawajibisha juu ya madai hayo huku pia ukitoa misaada ya kibinadamu kwa kiwango cha juu iwezekanavyo. "Ni muhimu kuheshimu uhuru wa mipaka ya Syria na kufanya juhudi za kutuliza hali ili watu wanaotaka kurudi nyumbani waweze kurejea. Tunapaswa kuwa waangalifu kwani Syria inaweza kuwa kiini cha mzozo wa kikanda. Kwa hivyo, tunasisitiza kusimamisha vurugu na kuheshimu uhuru wa nchi hiyo."
Soma pia: Viongozi wa EU kujadili mustakabali wa utawala mpya Syria
Viongozi hao wanakukutana mjini Brussels kwa mara ya kwanza tangu kuondolewa madarakani Rais Bashar al-Assad katika wakati mataifa wanachama wa umoja huo yakikabiliwa na maamuzi kuhusu jinsi ya kushughulika na kundi Hayat Tahrir al-Sham, lenye mamlaka ya uongozi kwa sasa na ambalo Umoja wa Mataifa unalitazama kama shirika la kigaidi na likikabiliwa pia na vikwazo vya umoja huo.