1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Jeshi lafunga uwanja wa ndege, barabara mjini Aleppo

30 Novemba 2024

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 13 nchini Syria vimeibuka tena baada ya waasi kushambulia ghafla mji wa Aleppo, moja ya miji mikubwa na kituo cha biashara cha kale nchini humo.

https://p.dw.com/p/4nb4f
Syria I Wapiganaji wakiwafyatulia risasi wanajeshi wa jeshi la Syria katika wilaya ya Rashidin nje kidogo ya mji wa Aleppo
Wapiganaji wakiwafyatulia risasi wanajeshi wa jeshi la Syria katika wilaya ya Rashidin nje kidogo ya mji wa AleppoPicha: Bakr Alkasem/AFP

Serikali ya Syria imeufunga uwanja wa ndege wa Aleppo na barabara zote zinazoingia katika mji huo leo Jumamosi, baada ya waasi wanaompinga Rais Bashar al-Assad kusema wamefika katikati mwa mji huo wa pili kwa ukubwa.

Wapiganaji hao wa upinzani wakiongozwa na kundi la Hayat Tahriri al-Sham, HTS, walifanya mashambulizi ya kushtukiza na kuteka maeneo na miji inayodhibitiwa na serikali wiki hii na kufika Aleppo, karibu muongo mmoja baada ya kulaazimishwa kuondoka huko na Assad na washirika wake.

Soma pia: Waasi wa Syria waingia Aleppo katika mashambulizi mapya dhidi ya Assad

Urusi ambayo ni mshirika muhimu wa Assad, imeiahidi Damascus msaada zaidi wa kijeshi kuwadhibiti waasi, zimesema duru mbili za kijeshi, na kuongeza kuwa zana mpya zingeanza kuwasili katika saa 72 zijazo.

Jeshi la Syria limeamriwa kufuata maagizo ya "kuondoka kwa usalama" kutoka maeneo makuu ya mji ambako waasi wameingia.