1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Watu 100 wajeruhiwa kwenye shambulizi la Urusi

19 Agosti 2023

Urusi imefanya shambulio kwenye mji wa Ukraine wa Chernihiv, ambao ni makao makuu ya mkoa wa kaskazini mwa nchi hiyo wenye jina sawa na hilo.

https://p.dw.com/p/4VM2M
Ukraine | Urusi
maafa ya shambulizi la ChernihivPicha: VALENTYN OGIRENKO/REUTERS

Urusi imefanya shambulio kwenye mji wa Ukraine wa Chernihiv, ambao ni makao makuu ya mkoa wa kaskazini mwa nchi hiyo wenye jina sawa na hilo.

Wizara ya mambo ya ndani ya Ukraine imesema shambulio hilo, limesababisha vifo vya watu 7 na kuwajeruhi wengine 100. Mji huo ulioko kilometa takriban 150 kaskazini mwa mji mkuu wa Kiev kuelekea Belarus, kwa kiasi kikubwa haukuwa umelengwa na mashambulizi mazito kuanzia miezi ya kwanza ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Shambulio hilo limetokea baada ya rais Vladimir Putin kufanya ziara ya nadra na kukutana na makamanda wanaoongoza oparesheni za kijeshi nchini Ukraine katika mji wa Rostov-on-Don ulioko kusini mwa Urusi, huku mwenzake wa Ukraine Volodymry Zelensky naye akizuru Sweden. Rais Zelensky amelaani shambulio hilo, ambalo amesema liliyalenga majengo, ukiwemo ukumbi wa burudani na chuo kikuu.