MigogoroMashariki ya Kati
Watu 16 wajeruhiwa Tel Aviv kwa kombora lililotoka Yemen
21 Desemba 2024Matangazo
Jeshi la Israel limesema lilishindwa kulizuia kombora hilo, ambalo lilipiga katika mji huo mkuu wa kibiashara na kuwalazimu wakaazi wengi kuzikimbia nyumba zao.
Waasi wa Houthi wa Yemen wamedai kuhusika na shambulio hilo, wakisema walitumia kombora la masafa marefu "wakiyalenga maeneo ya kijeshi ya Israel."
Mara kadhaa waasi hao wanaoungwa mkono na Iran wamekuwa wakifanya mashambulizi ya makombora dhidi ya Israel wakilenga kuonesha na Wapalestina tangu kuanza kwa vita vya Gaza zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Kufutatia shambulizi hilo la Tel Aviv, Israel imeyapiga maeneo kadhaa ndani ya Yemen ikiwemo bandari na vituo vya nishati vinavyosimamiwa na Wahouthi.