1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Waziri mkuu wa Syria akiri, nchi yake haina fedha za kigeni

11 Desemba 2024

Mohammed al-Bashir amekiri kwamba pamoja na lengo lake la kutaka kuwalinda raia wote wa Syria na kuwapa huduma za msingi, itakuwa vigumu kufanya hivyo kwasababu nchi haina sarafu za kigeni.

https://p.dw.com/p/4o0sa
Mohammed al-Bashir, Waziri Mkuu mpya wa Syria
Mohammed al-Bashir, Waziri Mkuu mpya wa SyriaPicha: Stringer/SANA/AFP

Waziri mkuu mpya wa Syria Mohammed al-Bashir amewatolea mwito raia wote wa nchi hiyo waliokimbilia mataifa mbali mbali ya ulimwengu,warejee nyumbani, baada ya kuangushwa utawala wa Bashar al-Assad.

Hata hivyo amekiri kwamba pamoja na lengo lake la kutaka kuwalinda raia wote wa Syria na kuwapa huduma za msingi, itakuwa vigumu kufanya hivyo kwasababu nchi haina sarafu za kigeni.

Jumuiya ya Kimataifa bado inafuatilia kwa karibu hali inayojitokeza nchini Syria. Mawaziri wa Umoja wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanapanga kuujadili mgogoro wa Syria kesho mjini Berlin.

Wakati huo huo waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ameelekea Jordan na baadaye Uturuki kwa ajili ya kuzungumzia mgogoro huo.

Qatar imesema itafunguwa tena hivi karibuni ubalozi wake mjini Damascus.