Baerbock: EU inaendelea kufuatilia mchakato wa kisiasa Syria
4 Januari 2025Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amesema Umoja wa Ulaya utaendelea kufuatilia kwa karibu mchakato wa kisiasa nchini Syria na kuiunga mkono nchi hiyo ikiwa inaelekea kwenye mustakabali wa amani na uwazi.
Baerbock ameyasema hayo mjini Damascus Syria ambako yeye na waziri mwenzake wa Ufaransa Jean-Noël Barrot, walifanya ziara jana ijumaa kwa niaba ya Umoja wa Ulaya.
Waziri Baerbock ameongeza kuwa tathmini yake ya kwanza ni jamii iliyogawika nchini Syria lakini kuna matumaini ya uhuru baada ya miaka mingi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, mateso na unyonyaji.
Amesisitiza kwamba Umoja wa Ulaya hautoiunga mkono nchi hiyo ikiwa itekelezaji sheria zinazobinya haki za wanawake na jamii za makabila madogo katika jamii. Viongozi hao walikutana na kiongozi wa mpito wa Syria Ahmed al-Sharaa wakati wa ziara yao.