1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern warejea nyumbani

28 Mei 2013

Bayern Munich iliyotawazwa mabingwa wa msimu huu wa Bundesliga na mabingwa wa Ulaya, Champions League, warejea nyumbani bila shangwe kubwa na Borussia Dortmund yapokelewa kwa shangwe na mashabiki 10,000.

https://p.dw.com/p/18em6
Die Mannschaft des FC Bayern München kommt am 26.05.2013 auf dem Flughafen in München (Bayern) an. Vorne tragen Spieler Philipp Lahm (l) und Trainer Jupp Heynckes den CL-Pokal. Der FC Bayern München gewann am 25.05.2013 im Finale der UEFA Champions League gegen Borussia Dortmund mit 2:1. Foto: Peter Kneffel/dpa +++(c) dpa - Bildfunk+++ pixel
FC Bayern Munich wakiwasili mjini MunichPicha: picture-alliance/dpa

Bayern ilirejea jana jioni(26.05.2013) mjini Munich bila ya sherehe kubwa, hii ikiwa ni mkakati wa kujitayarisha na fainali ya kombe la shirikisho, DFB Pokal ambalo litafanyika katika uwanja wa Olimpiki mjini Berlin dhidi ya VFB Stuttgart.

Kocha anayeondoka Jupp Heynckes na kapitano Philipp Lahm walibeba kwa pamoja kombe hilo wakati wakiteremka kutoka katika ndege iliyowaleta kutoka London hadi katika zulia jekundu kwa heshima ya timu hiyo bingwa, huku kukiwa na hali ya upepo mkali na mvua.

LONDON, ENGLAND - MAY 25: Head Coach Jupp Heynckes of Bayern Muenchen holds the trophy after winning the UEFA Champions League final match against Borussia Dortmund at Wembley Stadium on May 25, 2013 in London, United Kingdom. (Photo by Martin Rose/Getty Images)
Jupp Heynckes akiwa na kombe la Champions LeaguePicha: Getty Images

Kizazi cha dhahabu

Nahodha ya Bayern Philipp Lahm amesema kuwa huu ulikuwa ushindi muhimu kwa kundi la wachezaji wa timu hiyo ambao amewaita kuwa ni "kizazi cha Dhahabu."

"Ukiwa miongoni mwa kile kinachojulikana kama 'Kizazi cha dhahabu' , ni muhimu kushinda taji la kimataifa. Tumekwisha shinda mataji makubwa na kikosi hiki pamoja na kombe la shirikisho, lakini taji la kimataifa , ndio linalotambulika zaidi na mchezaji hutaka kushinda taji kama hilo, kama anachezea katika timu kubwa. Na hilo ndio hatimaye hii leo tumeweza kulifanikisha.

Munich's president Uli Hoeneß seen on the stands during the UEFA soccer Champions League final between Borussia Dortmund and Bayern Munich at Wembley stadium in London, England, 25 May 2013. Photo: Peter Kneffel/dpa
Nahodha wa Bayern Philipp LahmPicha: picture-alliance/dpa

Naye kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Löw alipoulizwa kuhusu mchezo huo wa fainali siku ya Jumamosi alielezea kuwa ni mafanikio ya soka katika Ujerumani.

"Kwanza kabisa ni soka ya Ujerumani iliyoonyeshwa. Na pia ni matokeo ya mambo mengi mazuri, ambayo yamefanyika katika miaka iliyopita. Kuhusu hilo tunastahili hasa kufurahi. Na hali hii ni nzuri kwa ajili ya hapo baadaye. Timu ya taifa na kocha wake kwa hiyo , wanapata mbinyo mkubwa kwa kila mashindano. Kwa hiyo naweza kuelewa , kwanini Wajerumani wanahamu kubwa kupata ushindi katika timu yao ya taifa.Na kwa hiyo tutafanya kila liwezekanalo."

Germany's national soccer coach Joachim Loew gestures during a news conference before their Euro 2012 soccer match against Italy in Gdansk, June 26, 2012. REUTERS/Thomas Bohlen (POLAND - Tags: SPORT SOCCER)
Joachim Löw kocha wa Die MannschaftPicha: Reuters

Borussia

Nahodha wa Borussia Dortmund Sebastian Kehl alikuwa na maneno ya kujipa moyo na kuueleza mchezo wa fainali kati ya timu hiyo yenye wachezaji chipukizi kuwa ulikuwa na nafasi sawa na kwamba Borussia inajivunia kila ilichokifanya msimu huu.

"Nafikiri , tumecheza vizuri sana. Tulianza vizuri sana, katika kipindi cha kwanza tuliwadhibiti kabisa Bayern, lakini tulipaswa kupata bao. Nafikiri hilo ndio lilikuwa ufunguo wa yote, kwa kuwa hali hiyo haikutokea. Na hatimaye Bayern iliwaangukia bahati na ilikuwa mwishoni mwa mchezo na nafikiri pia wamekuwa washindi kwa bahati. Tumecheza vizuri na tumejitangaza vizuri duniani na kwa hilo tunastahili kujivunia, kwa kile tulichokionesha leo."

Mabingwa wa Ulaya Bayern wanapanga pia kulitia kibindoni taji la ubingwa wa kombe la shirikisho, DFB Pokal Jumamosi ijayo mjini Berlin ili kumpa mkono wa kwaheri kocha wake aliyeleta mafanikio makubwa msimu huu Jupp heynckes kwa kudhamiria kubeba mataji matatu katika msimu huu.

Mbinyo kwa Guardiola

Hali hiyo hata hivyo inaonekana kutoa mbinyo mkubwa kwa kocha mtarajiwa wa Bayern Pep Guardiola. Kocha wa zamani wa Barcelona Pep Guardiola mwenye umri wa miaka 42 atajiunga na mabingwa hao wapya wa Champions League Juni 26 mwaka huu wakati Heynckes atakapokamilisha mkataba wake wa miaka miwilikwa pambano la DFB Pokal dhidi ya VFB Stuttgart.

Wakati huo huo Jupp Heynckes anatarajiwa kukubali ombi la kurejea katika klabu ya Real Madrid. jupp Heynckes mwenye umri wa miaka 68 aliiongoza Real madrid katika ubingwa wa Ulaya mwaka 1998 na pia aliwahi kuzifunza timu za Athletico Bilbao na Tenerife.

Two fans of Dortmund look dejected after the UEFA soccer Champions League final between Borussia Dortmund and Bayern Munich at Wembley stadium in London, England, 25 May 2013. Photo: Andreas Gebert/dpa
Wapenzi wa Dortmund wakitafakari kipigo dhidi ya BayernPicha: picture-alliance/dpa

Baada ya Bayern kunyakua taji la ubingwa katika Champions League dhidi ya klabu nyingine ya Bundesliga katika fainali kali iliyochezwa mjini London katika uwanja wa Wembley , lengo jingine la Ujerumani katika nyanja ya kimataifa ni kunyakua kombe la dunia.

Taji la tano

Ushindi wa tano wa Bayern katika Champions League ulihitaji miaka 12 kabla ya kutimiza ndoto hiyo, Ujerumani ilishinda mara ya mwisho kombe la dunia mwaka 1990. Taji lake la mwisho pia lilipatikana katika uwanja wa Wembley pale Ujerumani iliponyakua ubingwa wa Ulaya mwaka 1996.

Soka la Ujerumani imebadilika kwa kiasi kikubwa , lakini Die Mannschaft, timu ya taifa ya ujerumani imeambulia patupu mara nne katika mashindano makubwa licha ya mchezo wa kufurahisha wa mashambulizi.

Neymar

kocha wa Barcelona na wachezaji wameukaribisha uamuzi wa nyota wa soka nchini Brazil Neymar wa kujiunga na mabingwa hao wa uhispania dhidi ya mahasimu wao Real Madrid. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21 anatarajiwa kutia saini mkataba wa miaka mitano leo.

ARCHIV - Der brailianische Torschütze Neymar jubelt nach seinem Treffer in einem Freundschaftsspiel Schottland gegen Brasilien im Emirates-Stadion in London, Großbritannien (Archivfoto vom 27.03.2011). Am Mittwoch spielt die brasilianische Nationalmannschaft gegen Deutschland, und die größte Attraktion beim fünffachen Weltmeister ist der neue Wunderstürmer Neymar. Fast alle Großclubs jagen den 19 Jahre alten Stürmer - den Zuschlag erhält nun wohl Real Madrid. Foto: EPA/GERRY PENNY NO ONLINE ORINTERNET USE WITHOUT LICENCE FROMTHE FOOTBALL DATA CO. LTD. (zu dpa-KORR: "Alle wollen Neymar: Wunderkind vor Wechsel zu Real" vom 08.08.2011) +++(c) dpa - Bildfunk+++ pixel
Mchezaji Neymar atakayejiunga na BarcelonaPicha: picture alliance/dpa

Nayo Paris St. Germain ya Ufaransa ambayo imepata ubingwa wake wa kwanza baada ya muda wa miaka 19, ina matumaini kwamba msimu huu wa 2012-13 unaanzisha kipindi cha udhibiti wa soka la nchi hiyo kama ilivyokuwa kwa Olympique Lyonnais katika muongo mmoja uliopita.

Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe /ape / rtre

Mhariri: Mohammed Khelef