1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu: Wanajeshi watabakia ukanda salama na Syria

18 Desemba 2024

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema vikosi vya nchi yake vitaendelea kulikalia eneo la mpakani na Syria lisiloruhusiwa shughuli zozote za kijeshi hadi upatikane utaratibu mwingine wa usalama kwa Israel.

https://p.dw.com/p/4oHSf
Vikosi vya Israel
Vikosi vya Israel.Picha: Matias Delacroix/dpa/AP/picture alliance

Netanyahu ametoa matamshi hayo jana akiwa juu ya kilele cha mlima Hermon ulio ndani ya ardhi ya Syria unaopatikana umbali wa karibu kilometa 10 kutoka kwenye mpaka wa Israel.

Ukanda salama kati ya Israel na Syria ambao Netanyahu amesema wanajeshi wake watabakia, ulianzishwa na Umoja wa Mataifa mwaka 1974 kwa lengo la kuzingetanisha kijeshi nchi hizo mbili.

Vikosi vya Israel viliingia kwenye eneo hilo mnamo siku za karibuni baada ya kuungushwa utawala wa Rais Bashar al- Assad wa Syria.

Uamuzi huo wa Israel kupeleka wanajeshi wake na kulikalia eneo hilo umezusha ukosoaji mkubwa, wengi wakiituhumu nchi hiyo kukiuka makubaliano ya mwaka 1974 na kutumia hali ya msukosuko unaikabili Syria kujitwalia kipande cha ardhi.