1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Urusi yashambulia miundombinu ya nishati ya Ukraine

13 Desemba 2024

Urusi imefanya mashambulizi makubwa kwenye vituo vya nishati vya Ukraine, Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati wa Ukraine Galushchenko.Ukraine imetoa mwito kwa washirika wake wa kupatiwa mifumo zaidi ya ulinzi wa anga.

https://p.dw.com/p/4o692
Ukraine
Miundombinu ya nishati ya umeme inakabiliwa na mashambulizi ya UrusiPicha: Ed Ram/Getty Images

     
Urusi imefanya mashambulizi makubwa kwenye vituo vya nishati vya Ukraine, Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati wa Ukraine Galushchenko. Mashambulizi hayo yanafanyika wakati Ukraine ikiendelea kutoa mwito kwa washirika wake wa kupatiwa mifumo zaidi ya ulinzi wa anga.

Akitumia mtandao wa Facebook, Waziri wa Nishati wa Ukraine, Galushchenkoamesema kwa mara nyingine adui yao Urusi ameendeleza mashambulizi ya kutisha. Sekta nzima ya nishati ya Ukraine inakabiliwa na mashambulizi makubwa.

Soma zaidi. Scholz ahimiza kampuni kuwekeza zaidi nchini Ukraine

Mifumo ya nishati ya Ukraine tayari ilikuwa imeshambuliwa kwa mara ya kumi na moja na Urusi mwaka huu pekee na mashambulizi hayo yamesababisha uharibifu mkubwa na kukatika kwa umeme kwa muda mrefu kote nchini humo.

Kwa mujibu wa shirika la nishati la Ukraine,  Ukrenergo ni kwamba hata shambulizi la leo Ijumaa  limepelekea baadhi ya watu nchini humo kukosa huduma ya umeme.

Usiku wa kuamkia leo kelele za mifumo ya ulinzi wa anga zilishamiri katika maeneo mengi ya Ukraine kuashiria mashambulizi ya anga.

Baadaye mamlaka ziliripoti kutokea kwa milipuko mingi katika eneo la kusini mwa mji wa Odesa na katika maeneo ya mji mkuu Kyiv ambapo mifumo hiyo ya ulinzi wa anga ilikuwa ikifanya kazi.

Rais wa Ukraine
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyyPicha: IMAGO/ZUMA Press Wire

Kwa upande wake Rais Zelenskyy alipotembelea kambi ya kijeshi ya Zaporizhzhia amesema atazungumza na washirika wake wa magharibi ili kuongeza mifumo zaidi ya ulinzi wa anga.

Ukraine: Tunahitaji msada zaidi wa mifumo wa ulinzi.

Katika ujumbe wake wa kuwapongeza wanajeshi wake wanaopambana na vikosi vya Urusi,  Zelenskyy amesema...

Volodymyr Zelenskyy amesema  "Salamu, Waukraine wapendwa! Leo, nilikuwa Zaporizhzhia, eneo hilo. Ni Siku ya Vikosi vya Ardhini  Nimewapongeza askari wetu na kuwatunuku. Kikosi cha 65, Brigade ya 27 na madaktari wetu wa Kiukreni, mimi niwashukuru sana nyote na kwa hatua muhimu katika mwelekeo mzuri wa eneo la Zaporizhzhia, Asanteni kwa taaluma yenu, asante kwa kuilinda Ukraine na watu wetu''.

Soma zaidi.Mawaziri wa Ulaya kujadili uungaji mkono kwa Ukraine 
Mwito huo wa kuomba msaada zaidi wa mifumo ya ulinzi wa anga umetiliwa mkazo pia na Waziri wake wa mambo ya nje Andrii Sybiha akisema kwamba nchi yake inahitaji msaada wa haraka sana ili kukabiliana na mashambulizi ya Urusi yanayoendelea na ambayo yanalenga mifumo ya nishati ya umeme ya nchi hiyo hasa katika kipindi hiki cha msimu wa baridi.

Mashambulizi hayo ya Urusi kwenye miundombinu ya nishati ya Ukraine yamekuwa yakisababisha kukatika kwa umeme nchini humo.