You need to enable JavaScript to run this app.
Nenda kwenye maudhui
Nenda kwenye orodha kuu
Nenda tovuti zaidi za DW
Vidio zetu
Sauti zetu
Maeneo
Tanzania
Kenya
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Afrika
Ulaya
Mada
Haki za binadamu
Mazingira
Afya
Teknolojia
Kategoria
Matukio ya Kisiasa
Masuala ya Jamii
Michezo
Yanayoangaziwa
Uchaguzi Mkuu wa Ujerumani 2025
Mzozo wa Israel na Hamas
Bundesliga
Sauti zetu
Vidio zetu
Matangazo
Picha: DW
Picha: DW
Vidio zetu
Tazama vidio zetu hapa
Ruka sehemu inayofuata Maudhui yote kwenye mada hii
Maudhui yote kwenye mada hii
Mfahamu Aika mpishi maarufu wa supu ya kongoro Moshi
Aika Isaya ni mjarisiamali ambaye anakidhi maisha yake kwa biashara ya supu na vinywaji vya moto. Miongoni mwa supu ambazo hupikwa hapo , supu ya kongoro ndio hupendwa zaidi, na wateja hupenda kupata supu hiyo na kitafunwa cha chapati. #kurunziwanawake
Mlipuko wa virusi vya Rota mjini Mombasa
Jiji la Mombasa nchini Kenya limekumbwa na ,lipuko wa Rotavirus, ugonjwa unaosababisha kutapika na kuharisha miongoni mwa watoto. Je, Rotavirus inatokana na nini na nini tiba yake?
Maonyesho ya viwanda ya Hannover yarejea na azma ya kuendeleza Akili Bandia-AI
Makampuni zaidi ya 4000 yanamulika teknolojia yao mpya katika maonyesho makubwa kabisa ya teknolojia ya viwanda yaliyoanza Jumapili mjini Hannover, Ujerumani. Dira wanayoiangazia ni maendeleo ya akili bandia kama suluhisho kwa matatizo mengi yanayoikumba dunia ya leo. #Kurunzi
Maoni ya wakaazi wa Goma juu ya vikosi vya Jumuiya ya Afrika Mashariki
Maoni ya wakaazi wa Gomba juu ya vikosi vya Jumuiya ya Afrika Mashariki
Roboti "Da Vinci" lapandikiza mapafu kwa binadamu.
Kwa mara ya kwanza, hospitali moja nchini Uhispania imeweza kupandikiza mapafu ya binadamu kwa kutumia mbinu ya upasuaji wa roboti aliyepewa jina la "Da Vinci". #kurunziafya
Mapigano mapya yaua watu takribani 100 Sudan
Mji mkuu wa Sudan wa Khartoum unakabiliwa na siku ya tatu ya mapigano makali kati ya makundi pinzani ya jeshi yanayopambana kudhibiti nchi. Kurunzi
Elimu kwa Warohingya bado kitendawili
Wakimbizi wa Rohingya wengi wao wanaoishi nje ya Myanmar bado wanakabiliwa na hali tete. Wengi bado hawahisi kama wako salama, na kupata elimu kwao bado ni kitendawili. Basi hii leo, kutana na binti huyu aliyepambana kimasomo hadi kupata shahada ya kwanza. Njia haikuwa nyepesi hata kidogo. Tizama video hii kwa mengi zaidi. #Kurunziwanawake
Kibanda mwendo chawezesha wakulima wa Arusha kuuza mboga na matunda freshi
Juhudi bila maarifa wakati mwingine huwa ni kazi bure. Chukua mfano wa muuza mboga na matunda ambaye hana mbinu za kuzifanya bidhaa zake ziendelee kuwa freshi, baada ya muda mfupi zitaharibika. Kwa wachuuzi wa mjini Arusha, jibu limepatikana kutokana na kibanda-mwendo. Kuelewa zaidi, tazama vidio hii iliyoandaliwa na mwandishi wa DW mjini Arusha, Veronica Natalis. #Kurunzi
Wanawake wajitosa katika ubebaji wa samaki soko la Feri
Kazi ni kazi na mchagua jembe si mkulima ni miongoni mwa misemo inayohamasisha watu kutodharau au kubagua kazi, kwa sababu ukifanya hivyo matokeo yake ni umasikini na utegemezi kwa watu wengine. Misemo hii inawahusu wanawake walioamua kuizamia kazi ya kubeba samaki kwenye soko la Feri jijini Dar es Salaam, na kujipatia kipato kinachoambatana na heshima ya utu. #Kurunzi
Dada mwendesha baiskeli Kenya anayetaka kushindana kimataifa licha ya kuwa kiziwi
Kutana na Monica Wambui, anayeshiriki mashindano ya kuendesha baiskeli na ambaye ana ulemavu wa kusikia. Ameshinda umaskini na ukosefu wa nyenzo muafaka za kushinda mashindani ya uendeshaji baiskeli. Hata mazingira ya mazoezi kwake wakati mwingine huwa hatari.
Madhara ya kuvaa viatu virefu
Unafahamu kuwa viatu virefu vina madhara kiafya? Kufahamu zaidi fuatana nasi hapa umsikie mtaalamu akifafanua zaidi katika video hii ya Kurunzi ya Afya.
Msichana Jasiri-Asia Mussa , binti wa mjini anayefanya ufundi wa magari
Wahenga walisema mchagua jembe si mkulima, na kazi ni kazi mradi mkono uende kinywani. Binti Asia Mussa wa Dar es Salaam ameamua kuwa badala ya kukimbizana na kazi za kuajiriwa, afuate ndoto zake, akakunja mikono ya shati na kuzamia katika umakenika wa magari. Na huo ni mwanzo tu. Sikiliza hadithi yake, na pia ndoto zake katika vidio hii ya #MsichanaJasiri.
Mina Guli, mwanaharakati anayetumia mbio kuhamisisha utunzaji wa maji
Sio watu wengi wakiulizwa ipi ni raslimali muhimu kwa maisha ya viumbe hai, watajibu ni maji. Ukweli lakini ni kuwa maji ni nguzo ya maisha duniani, na matumizi mabaya ya raslimali hiyo yanaiweka hatarini. Ni kwa sababu hii Mina Guli aliacha kazi nyingine na kuwa mwanaharakati anayehamasisha walimwengu juu ya umuhimu wa maji, kwa kutumia mbio zinazompeleka katika sehemu nyingi za dunia. #Kurunzi
Blue Earth inavyotunza mazingira Mombasa
Wasiwasi wao kuhusu mabadiliko ya Tabianchi uliwasukuma kuchukua hatua ili kutoa mchango kupambana na changamoto hiyo, hivi sasa shirika la Blue Earth lililoasisiwa na wanawake watatu mjini Mombasa, linafanya zaidi ya kupanda mikoko katika harakati zake za uhifadhi wa mazingira. Ni #kurunziwanawake iliyoandaliwa na Ripota wetu wa Mombasa Fathiya Omar.
Msichana Jasiri: Mfahamu Madeeha Ghulam na harakati zake
Maddeha Ghulam ni binti anayemulikwa safari hii kwenye makala hii maalumu kabisa ya wasichana wanaoamua kuchukua hatua za kuisaidia ama kuinusuru jamii na mengine yanayozunguka jamii hizo. Ni nani hasa huyu bintiß Sikiliza makala haya.
Msichana wa miaka 13 anamiliki kiwanda cha sabuni
Umri si kigezo cha uthubutu haya yanadhihirishwa na msichana mgogo aliyejifunza ujasiriamali na bidhaa zake zipo sokoni
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu afanya ziara Berlin
Sehemu za Berlin zilifungwa huku polisi wakionekana kuwa tayari kukabiliana na maandamano dhidi ya ziara ya Netanyahu.
Mwanamke anayetoa elimu ya uzazi kwa wasichana
Katika Kurunzi Wanawake leo tunamuangazia Beatrice Magani anayetoa elimu sahihi ya masuala ya uzazi kwa vijana wa kike. Amefanikiwa wasichana wengi kupitia vikundi ambavyo vinatengenezwa na vijana wenyewe katika maeneo mbalimbali hasa yale ya vijijini.
Uongozi na motisha kwa wafuasi
Zuwena Mohammed anajulikana kama Shilole, anaongoza wafuasi zaidi ya milioni 10 kwenye mitandao ya kijamii,
Makumbusho inayotembea Tanzania
Makumbusho ya taifa Tanzania inaendesha mradhi wa makumbusho inayotembea, dhima ni kuwafikia watu wengi zaidi
Msichana Jasiri kutoka Marsabit, Kenya
Katika kipindi cha Msichana Jasiri, Michael Kwena anamuangazia Jillo Fugicha, Msichana Jasiri kutoka Marsabit, nchini Kenya ambaye ameanzisha Shirika la kijamii la kupambana dhidi ya Ukeketaji.
Jasiri anaeamini juu ya elimu ya mazingira kwa jamii
Si kila mmoja anaweza kuthubutu kuhusu kuyatunza mazingira lakini kwa jasiri Upendo amethubutu zaidi kwa kuamini elimu pekee ndio suluhisho la kudumu katika kuyatunza mazingira na si elimu tu, bali kuwaelimisha watoto na wanawake kuhusu mazingira bora na ustawi wake.
Msichana Jasiri: Mtafsiri wa lugha ya alama
Makala hii ya Msichana Jasiri inamwangazia Halima Salim, binti anayejitolea kutafsiri lugha ya alama kwa wanafunzi wenzake ambao ni viziwi kwenye shule ya sekondari ya Mtwara Ufundi iliyoko mkoani Mtwara kusini mwa Tanzania. Msikilize Salma Mkalibala akisimulia.
Tiba ya vitendo kwa waathirika wa dawa za kulevya
Tiba ya vitendo kwa waathirika wa dawa za kulevya
Msichana Jasiri: Msichana anayetoa elimu shuleni na vyuoni juu ya kujitambua
Katika umri wa miaka 19 tu swaiba anathubutu kupita shuleni pamoja na vyuoni kuitoa elimu kwa wasichana wengine juu ya kujitambua. Hii si rahisi kwake lakini nguvu nyingi na masaada wake mkubwa unatoka katika jamii. Si rahisi kwa jamii yake kumuelewa lakini matumaini yake ni kuwafikia wasichana wengi na anatamani kuona wazazi wanaotoa elimu madhubuti juu ya kujitambua kwa vijana wao.
Akina mama na ujumbe wa amani Mombasa
#KurunziWanawake leo inamulika wanawake wa Mombasa, Kenya ambao wametumia maonyesho ya utamaduni wa wapwani kueneza ujumbe wa amani kwa kauli mbiu ya “Amani ni Mama na Mama ni Amani“. Vidio ya mwandishi wetu wa Mombasa Halima Gongo inaeleza juhudi hizo. #kurunziwanawake
Fahamu dalili za awali za mtoto mwenye maradhi ya moyo
Takwimu mbali mbali zikiwemo za Shirika la Afya Ulimwenguni ,WHO, zinaonesha kuwa watoto wengi hufariki kabla ya mwaka mmoja kwa ugonjwa wa moyo bila kugundulika na kupatiwa matibabu ya haraka. Kurunzi afya inaangazia dadili za awali za ugonjwa huo kwa watoto.#Kurunzi Afya
Sarakasi ya Mekele yaanza kurejea baada ya vita
Vita katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia vilivuruga ndoto za wanasarakasi vijana. Lakini kwa sasa kadri makubaliano yanavyozidi kuheshimiwa, ndivyo sarakasi maarufu ulimwenguni ya Mekele inavyozidi kurejea.
Msichana Jasiri: Rubani ambaye pia anatengeneza udi
Wadh- hat ni rubani ambaye ameamua kuwafundisha watu jinsi ya kutengeneza udi ili kujikwamua na janga la ukosefu wa ajira. Kwake haikuwa rahisi kwa sababu watu wa jamii yake waliamini kuwa udi bora hutoka katika mataifa ya Uarabuni. Lakini sasa amekuwa ni msaada kwa baadhi ya watu na hata wengine kumuona kuwa daraja kwao katika kuyafikia malengo yao.
Ubunifu wa kutengeneza samani kwa Kamba Dar es Salaam
Utengezaji wa pembea na makabati kwa kutumia kamba ni njia moja ya kuwaingizia vijana kipato pamoja na kunusuru mazingira kinyume na bidhaa nyingi za aina hiyo ambazo huagizwa toka mataifa ya mbali. Tazama ubunifu wa vijana hawa mjini Dar es Salaam
Ujerumani na Tanzania waendeleza ushirikiano
Ujerumani na Tanzania waendeleza ushirikiano wa kimkakati
Mradi wa kukusanya taka wa Baus Taka Mombasa
Kurunzi Wanawake leo inammulika Tayba Hatimy, ambaye aliamua kuitumia changamoto ya taka kuzagaa hovyo katika mtaa wa Old Town, mjini Mombasa, Kenya kuanzisha mradi wa Baus Taka unaotumia programu ya simu ya mkononi kwa ajili ya kukusanya taka kwenye mji huo.
''Radio Generation'' yahamasisha usafi wa mji wa Abidjan
Wakati dunia ikisheherekea siku ya kimataifa ya redio, tunakimulika kituo kimoja cha huko Ivory Coast, Radio Generation, au ''Redio ya Kizazi Kipya'', ambacho redio yake ya mtandaoni inavyo vipindi mahsusi kwa ajili ya kuhamasisha usafi wa mazingira katika kitongoji kimoja cha mji huo, ambako wakaazi wake wanaishi katika mazingira machafu kabisa.
WHO yahofia magonjwa ya mripuko Uturuki na Syria
Wakati taarifa kutoka maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko kubwa la ardhi nchini Uturuki na Syria zikijikita juu ya vifo, majeruhi na uharibifu wa miji, shirika la afya duniani, WHO linaonya juu ya uwezekano wa kutokea kwa miripuko ya magonjwa ya kuambukiza. Linasema mazingira wanamoishi manusura wa tetemeko hilo ni changamoto kubwa.
Wakonta anatumia ulimi,teknolojia kuandika
Ajali alioipata haikuzuia kufikia malengo yake ya masomo na biashara, alijifunza kutumia viungo vilivyobaki katika lengo
Fatema:Nitapambania afya ya jamii yangu
Fatema Juma mwanamke alinaepambania afya ya jamii kwa kutoa elimu ya lishe na mazoezi ili kupunguza uzito uliopitiliza.Ameamua kujikita katika hilo kutokana na yeye kuwahi kukumbwa na tatizo hilo ambalo lilileta athari kwa familia yake.Tazama video
Siku ya Mitandao Salama, hali ikoje kwa vijana Tanzania?
Matumizi ya mitandao imekuwa sehemu ya maisha ya watu wengi. Japo kuna faida nyingi, athari pia zipo na ndiyo sababu kila mwaka kuna kampeni ya kuhamasisha mitandao salama. Baadhi ya vijana hawa kutoka Tanzania wanaelezea manufaa na athari ya mitandao kwao.
Miaka 60 na mchango wa maudhui ya vijana
Tunaadhimisha miaka 60 ya upashaji habari maudhui ya vijana ni kipaumbele chetu.Vipi yamewanufaisha kufikia malengo yao?
Huduma ya Bima ya Afya kwa wote
Bima ya Afya kwa wote ni chachu ya maendeleo, ingawa huduma hiyo imeendelea kuwa tatizo kubwa katika bara la Afrika. Tazama video hii fupi kutoka kwa mwandishi wetu Veronica Natalis ambayo inaangazia iwapo wananchi wako tayari kulipa kwa hiari bima yako ya afya na wanatarajia nini kutoka katika bima yao? Na pia inaangazia utaratibu upi utafaa kusaidia huduma ya bima ya afya kufika kwa wote.
Jasiri katika kilimo biashara
Alipoanza kilimo biashara familia haikumuelewa lakini kadri alivyoamua kuongeza bidii katika kile anakiamini, sasa anafurahia hatua anazopiga. Anamiliki kiwanda kidogo kuchakata viungo vya kupikia
Je, unadhani vifaa vya kisasa vimepoteza ladha ya mziki?
Je, unadhani vifaa vya kisasa vimepoteza ladha ya mziki?
Puto la tumbo la chakula ili kupunguza unene
Tiba: Puto la tumbo la chakula ili kupunguza unene
Fahamu ndoto za Witness Raphael mlimbwende wa viti mwendo
Msichana aliyethubutu kuwania mashindano ya ulimbwende wa viti mwendo Duniani , safari yake haikuwa rahisi lakini uthubutu wake umekuwa na manufaa na kuwa mfano kwa wasichana na vijana wengine. Anatamani kuona jamii yenye usawa haswa kwa watu wenye changamoto za kimaumbile kujitokeza na kutumia vilivyo vyao ili kuziishi ndoto zao.
Jasiri kwa wasio na makaazi
Ayshat msichana anayelikusanya kundi la watoto lililosahaulika na kuwapatia mahitaji yao muhimu huku akiwa akitamani kuona jamii yenye usawa na anatamani kuona jamii inalikumbuka kundi hili.Tazama video
Kazi ni kazi, haina mwenyewe!
"Hapa kazi tu", pengine ndivyo anavyosema mwanamama huyu anayeongoza uzalishaji kwenye kiwanda cha chaki. Kuna mengi ya kujifunza hapa. Tafadhali tizama video hii kwanza, kisha utuambie. #Kurunzi.
Pele, kiboko ya mabeki
Rais mpya wa Brazil Lula da Silva amewaongoza maelfu ya waombolezaji kutoa heshima zao za mwisho kwa Pele.
Umewahi kubebwa kwa daladala za baiskeli?
Umewahi kubebwa kwa daladala za baiskeli?
Ukurasa uliotangulia
Ukurasa 6 wa 6
Ukurasa unaofuatia