Marekani: Mazungumzo ni chanya na kiongozi mpya wa Syria
21 Desemba 2024Matangazo
Marekani iliwatuma mjini Damascus wadiplomasia wake wawili Barbara Leaf, anayeshughulikia masuala ya Mashariki ya Kati na Roger Carstens ambaye ni mjumbe maalum wa masuala ya mateka kuzungumza na Al-Sharaa aliyeongoza kundi la waasi la Hayat Tahrir al-Sham, kuuangusha utawala wa Rais Bashar Al-Assad wiki mbili zilizopita.
Leaf amewaambia waandishi habari kuwa mazungumzo yao yalituama juu ya umuhimu wa kuyadhibiti makundi ya kigaidi yasilete kitisho ndani na nje ya Syria.
Leaf amesema kufuatia mazungumzo ya kutia moyo, Marekani itaipatia Syria msaada wa dola milioni 10. Ziara ya wanadiplomasia hao wa Marekani ilikuwa ya kwanza tangu kuangushwa utawala wa Assad.