1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ucheleweshaji wa kura wazusha hasira Namibia

29 Novemba 2024

Namibia iliongeza muda wa kupiga kura kwa mara ya pili Alhamisi, huku upinzani ukilalamikia matatizo ya vifaa yaliyowazuia wapiga kura wengi kushiriki uchaguzi.

https://p.dw.com/p/4nY0h
Namibia | Uchaguzi Mkuu
Uchaguzi umesogezwa kwenye baadhi ya vituo hadi Ijumaa na JumamosiPicha: Simon Maina/AFP/Getty Images

Vyama vya upinzani vilitaka kusimamishwa kwa zoezi la kuhesabu kura na kusema kuwa wamepoteza imani na mchakato huo.

Uchaguzi huo ni mtihani kwa chama cha SWAPO ambacho kimetawala tangu uhuru miaka 34 iliyopita, na sasa kinakabiliwa na wapiga kura vijana waliokasirishwa na ukosefu wa ajira na usawa.

Soma pia:Namibia yarefusha muda wa upigaji kura kutokana na changamoto za uratibu 

Tume ya uchaguzi ya Namibia, ECN, iliahirisha muda wa baadhi ya vituo hadi Alhamisi na kuamua vituo 36 vikae wazi hadi Ijumaa na Jumamosi baada ya ukosoaji huo.

Pia ilikiri kuwepo kwa matatizo kama upungufu wa karatasi za kura na kuchemka kwa vifaa vya kielektroniki vya kuhakiki wapigakura. Chama cha upinzani IPC kiliongoza miito ya kusimamishwa kwa mchakato huo.